2024-10-11
Design
Architecture
Tarehe 11/10/2024, MYCN kupitia Wanahabari Watoto kwa kushirikiana na Baraza la Watoto la Kata ya Kahama, limeendesha zoezi la kutoa elimu kuhusu mabadiliko ya tabianchi na utunzaji wa mazingira kwa wanafunzi wa shule ya msingi Magaka. Zoezi hili limejumuisha upandaji wa miti zaidi ya 100 kwa ushirikiano na wanafunzi wa shule hiyo pamoja na walimu.
Shughuli hii imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali kutoka ngazi ya kata na halmashauri, wakiwemo Afisa Elimu Kata, Afisa Mtendaji Kata, Mwenyekiti wa Mtaa, Afisa Maendeleo ya Jamii, Afisa Afya, walimu wa shule hiyo, pamoja na Msajili wa Asasi zisizo za Kiraia, Mr. Yusuph Okoko, aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
Tunatumaini kwamba zoezi hili litachochea watoto kutunza mazingira na kuwa mabalozi wazuri wa mazingira katika jamii. Kama kaulimbiu ya watoto inavyosema, #Mazingira Stahimilivu kwa Ustawi wa Mtoto.
#ClimateAction #ElimuKwaWatoto
#maendeleoyawatotonavijana