MYCN

2025-06-16

Interior

Architecture

Villa

Design

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA 2025

siku-ya-mtoto-wa-afrika-2025

Leo MYCN tumeadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwa kishindo! πŸ§’πŸΎπŸ‘§πŸ½

Katika ukumbi wa Halimashauri, Manispaa ya Ilemela pamoja na katika Wilaya ya Nyamagana tumeungana na watoto, Wadau wa Maendeleo ya Watoto, Serikali pamoja na wananchi kwa kuadhimisha siku hii muhimu kwa kauli mbiu:

πŸ“’ "Haki za Mtoto: Tulipotoka, Tulipo na Tuendako."

Mgeni rasmi wa tukio alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela akimwakilisha Mkuu wa Wilaya, ambapo masuala mbalimbali muhimu kuhusu watoto yalijadiliwa, yakiwemo:

βœ… Haki za watoto

🚫 Mapambano dhidi ya ukatili kwa watoto

πŸ—£οΈ Sauti ya watoto kupitia Bunge la Watoto

🎭 Burudani za watoto (igizo, ngonjera, nyimbo)

❀️ Kuwashika mkono watoto wenye mahitaji maalum


Tunaamini kuwa kutoa nafasi kwa watoto kujieleza, kusikilizwa na kushirikishwa ni msingi wa kujenga jamii yenye usawa na haki.

Asante kwa wote waliohudhuria na kushiriki kutengeneza siku hii kuwa ya kipekee kwa watoto wetu! πŸ™ŒπŸΎ

Kwa pamoja, tunalinda, tunatetea, na tunaendeleza ndoto zao!

#SikuYaMtotoWaAfrika2025 #maendeleoyawatotonavijana